Muulize BizmarTZ

Mteja

Habari BizmarTZ, wewe ni nani?

Mimi ni system inayosimamia duka lako kidijitali — nakusimamia oda, stock na pesa kila zamu.

01 / 10
  • Oda zinakaguliwa kabla ya kutoka
  • Makabidhiano ya kila muuzaji
  • Unaona ukiwa popote
8Bidhaa zinazofanya kazi pamoja
5Majukumu — kila mtu na ruhusa yake
30Siku za kwanza bure
24/7Unaona duka lako ukiwa popote
Kazi za meneja

Kazi ambazo ungemlipa meneja — BizmarTZ inazifanya

  1. 01

    Inakagua kila oda

    Muuzaji anaandika oda kwa code yake; counter au jikoni linaipokea kabla haijatoka. Hakuna kinachotoka bila kuandikwa.

  2. 02

    Inalinda stock

    Kreti inaingia, chupa inatoka kwa mauzo. Hesabu ya stoo inaonyesha kilichopotea na thamani yake — mapema, si mwisho wa mwezi.

  3. 03

    Inapokea makabidhiano

    Kila muuzaji anaona cash na pesa za simu anazotakiwa kukabidhi; cashier anapokea kwa kubonyeza mara moja. Upungufu unaandikwa kwa jina lake.

  4. 04

    Inakuletea ripoti

    Faida kwa kila bidhaa, mauzo ya kila saa na mafungu ya pesa — unaona papo hapo, hata ukiwa nje ya mji.

Duka lako

Wewe furahia biashara — BizmarTZ inashika hesabu

Wateja wanaona counter, grill na burudani. Nyuma yake, BizmarTZ inasimamia kila chupa, kila mshikaki na kila shilingi — kama meneja asiyelala, bila daftari.

Bidhaa

Bidhaa za BizmarTZ

Kila kitu ambacho meneja makini angefanya kwenye duka lako — kimegawanywa katika bidhaa nane zinazofanya kazi pamoja.

Soma kila bidhaa
Pesa zinasimamiwa

Kila shilingi ina kazi yake

BizmarTZ inatenga pesa kabla hazijatumika: kila mauzo yanagawanywa kwa asilimia zako — TRA, kodi, mkopo, LUKU na kununua mzigo mpya — kama meneja makini angefanya.

  • Mmiliki
  • Kununua mzigo
  • Mfanyakazi
  • Kodi ya pango
  • TRA
  • Mkopo
  • LUKU
  • Matengenezo
  • Maji
  • Dharura
  • Mengineyo
Na zaidi

Meneja aliyejengwa kwa bar

Stock kwa Kreti na kwa Kilo

Bia inanunuliwa kwa Kreti na kuuzwa kwa Chupa, Nyama inanunuliwa kwa Kilo na kuuzwa kwa Mshikaki, Portion au Nusu — BizmarTZ anajua kila kipimo kinatoa kiasi gani Stoo.

Wauzaji kwa code yao

Kila Muuzaji anauza kwa Code na PIN yake, Bill na Commission zinaenda kwake.

Inafanya kazi bila Mtandao

Mauzo yanaendelea mtandao ukikatika, na kuhifadhiwa mtandao unaporejea.

Malipo ya Simu

Cash, M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money, HaloPesa na Benki yanapokelewa.

Bill na Risiti

Print bill kabla ya kulipa na risiti baada ya kulipa, kwenye printer ya 58mm.

Taarifa papo hapo

Oda ikitumwa inafika Counter au Jikoni hapo hapo: Bill ikilipwa kila skrini inasasishwa.

Kwa kila mtu

Kila mtu anaona kazi yake tu

Mmiliki

Faida, mafungu ya pesa na ripoti za matawi yote.

Meneja

Stock, hesabu ya stoo, wafanyakazi na upungufu.

Cashier

Kupokea malipo, makabidhiano ya wauzaji na cash-up ya zamu.

Counter na Chef

Kupokea au kukataa oda — vinywaji counter, chakula jikoni — kabla hazijatoka.

Muuzaji

Bill zake, oda zake na pesa anazotakiwa kukabidhi — kwenye simu yake.

Kazi inavyofanyika

Kuanza ni hatua nne

  1. 1

    Wasiliana nasi

    Tuambie kuhusu duka lako — matawi, bidhaa na wafanyakazi.

  2. 2

    Tunaweka duka lako

    Bidhaa, bei, mgawanyo wa pesa na code za bill zinawekwa tayari.

  3. 3

    Wafanyakazi wanaingia

    Kila muuzaji anapata code na PIN yake; cashier, counter, chef na meneja wanapata akaunti zao.

  4. 4

    Unasimamia ukiwa popote

    Ripoti, makabidhiano na stock zinakufikia kwenye simu yako kila siku.

Siku 30 bureKisha usajili wa kila mweziKila kitu kimo:
  • Bidhaa zote — oda, stock, makabidhiano na ripoti
  • Simu za wauzaji na kompyuta ya counter
  • Tunakusaidia kuweka duka lako
  • Unalipa kwa M-Pesa, Tigo Pesa au Airtel Money
Wasiliana kwa bei
Maswali

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

BizmarTZ anafanya kazi na Vifaa gani?

Anafanyakazi na Simu, Tablet au Kompyuta. Wauzaji wanatumia simu zao wenyewe.

Mtandao wa simu Ukikatika Bidhaa Itaendelea?

Ndio Itatolewa, Taarifa itatunzwa kwenye kifaa chako na kuhifadhiwa pindi mtandao unaporejea

Printer gani inafaa?

Printer ya risiti ya 58mm inayounganishwa na simu au kompyuta. Risiti inaweza pia kuonekana kwenye skrini bila kuchapishwa.

Muuzaji anaweza kutoa kinywaji bila kuandika?

Kila Oda inapita Counter au Jikoni kabla haijatoka, na stock inahesabiwa — Kinachokosekana kinaonekana kwenye Ripoti ya upotevu wa stock.

Maswali yote
Last call

Usiharibu Bar kwa kukosa Msimamizi. BizmarTZ ni Suluhisho.

Tuandikie tukuelezee zaidi, tukusaidie kuanza au tukusajilishe BizmarTZ kwa duka lako.

barnabachristopher@gmail.com